Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JUMLA
ya sh.100,400,000 zimekopeshwa kwa wajasiriamali wapatao 974 mkoani
Tabora kwa lengo la kuondoa umaskini na kuongeza ajira kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa na
Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) Mkoa wa Tabora
Samwel Neligwa ofisini kwake alipokuwa akizungumza na mwandishi wa
gazeti hili.
Alisema ili kufikia
lengo la shirika hilo la kuondoa umaskini pamoja na kukuza maendeleo ya
viwanda vidogo vidogo na biashara alisema SIDO imeweza kutoa mikopo hiyo
kwa wajasiriamali wa mkoa huo na hivyo kuongeza ajira 1,637.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2009/10 hadi 2013/14 mafunzo mbalimbali 228 yalitolewa kwa wajasiriamali wapatao 4,485.
Alieleza mkakati
mwingine unaofanywa na SIDO kuwa ni kuibua na kuendeleza bidhaa maalum
katika kila wilaya kwa kuzingatia malighafi na utaalam uliopo kwenye
wilaya husika.
Neligwa alisema lengo
la mkakati huo ni kuweza kuhamasisha wilaya husika kuchagua bidhaa
maalum itakayoweza kusaidia kuharakisha maendeleo ya kiuchumi kwa
wananchi.
Alisema uhamasishaji
huo hufanywa kwa kushirikiana na ofisi za wilaya na utekelezaji wake
hufanywa kwa kuunganisha nguvu na rasilimali zilizopo za SIDO na
serikali.
Aliyataja mazao
yanayopewa msukumo mkubwa katika mkakati huo unaofanyika katika wilaya
zote za Mkoa wa Tabora kuwa ni asali na nta, alizeti, mpunga, viatu na
bidhaa mbalimbali za ngozi.
Neligwa ameeleza kuwa
mkakati huo unaojulikana kwa jina la wilaya moja bidhaa moja (ODOP)
alisema umetoa fursa kubwa kwa vijana vijijini ambako ndiko walipo
vijana wengi kuweza kujiajiri kutokana na kuanzisha miradi na viwanda
vidogo na hivyo kusema hali hiyo imeweza kuleta matokeo makubwa kiuchumi
na kuongeza kipato na ajira kwa vijana.
Aliongeza kusema kuwa
hivi sasa tayari kuna wajasiriamali wa bidhaa za ngozi ambao baada ya
kuwezeshwa na SIDO wajasiriamali hao uzalishaji wao umeongezeka na hata
kufungua maduka ya viatu vya ngozi.
Alisema licha ya
wajasiriamali hao kuweza kujiajiri wenyewe lakini wameweza kuajiri pia
watu wengine baada ya kufungua maduka ambayo yapo Tabora mjini na
Igunga.
Neligwa alisema katika
programu ya kusaidia mafundi wanashirikiana na shirika lisilo la
kiserikali la Uingereza lijulikanalo kama TOOLS FOR SELFRELIANCE
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment