Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angella Kairuki
Huduma hiyo italenga kuwasaidia kesi za watoto, jinai, kufarakana kwa wanandoa, miradhi na urithi, ardhi, mikopo na ajira.
Mratibu wa kituo chicho, Goodluck Chuwa, alisema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa yake ya maandalizi ya kuanzisha kituo hicho kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angella Kairuki, aliyetembelea Taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam juzi.
Alisema huduma ya kisheria itatolewa na wanafunzi wanaofundishwa katika Taasisi hiyo bure, huku wakisimamiwa na walimu na mawakili wenye uzoefu.
“Wanafunzi hao hawataruhusiwa kutoa uwakilishi mahakamani. Bali watakuwa wakitoa huduma ya elimu, ushauri, uandishi wa nyaraka za kisheria, usuluhishi,” alisema.
Mkuu wa Taasisi hiyo, Jaji Gerald Ndika, aliishukuru serikali kwa kuongeza bajeti ya mikopo ya wanafunzi kufikia Sh. milioni 600.
“Hii inatuonyesha kuwa serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria inatujali. Kwa kuwa bila mikopo hatuwezi kupata wanafunzi 300 kwa muhula mmoja,” alisema.
Akijibu taarifa hiyo, Kairuki alisema serikali inaendelea kutafuta namna ya kutatua changamoto zinazoikabili Taasisi hiyo.
Alisema wizara yake inaendelea na mchakato wa kuandaa muswada wa sheria na kuufikisha kwenye baraza la mawaziri ili baadaye kupelekwa bungeni kwa ajili ya kuupitisha.
“Unajua tunakabiliwa na changamoto, kwa kuwa siyo kila kikao cha Bunge ni cha kupitisha sheria. Lakini mara baada ya kupitishwa kwa sheria hiyo, itawatambua wadau wote wanaotoa msaada wa kisheria ili kuwapatia motisha kwa kazi nzuri wanayoifanya,” alisema.
Alisema lengo la ziara ni kuangalia shughuli zinazofanywa na watoa msaada wa kisheria kwa wananchi na kujua changamoto wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment