Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WIZARA ya Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati, imewaagiza watu
wanaojishughulisha na uvuvi haramu kwenye bwawa la Mwanzugi, wilayani
Igunga, mkoani Tabora waache na endapo wataendelea kukaidi amri hiyo
hatua zitachukuliwa dhidi yao.
Ofisa uvuvi mfawidhi na uvunaji wa viumbe hai kanda hiyo, Renatus Karumbeta, alisema hayo katika mahojiano maalum na Tanzania Daima
baada ya kuwepo kwa malalamiko kwamba licha ya bwawa hilo kufungwa,
wapo wavuvi wanaoshirikiana na maofisa uvuvi kuvua nyakati za usiku.
Ofisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia ufugaji wa samaki katika mikoa
ya Dodoma, Singida na Tabora kuwa idara yake imeanza kupandikiza
samaki na mpaka sasa vifaranga 22,000 vya samaki vimepandikishwa katika
bwawa la kijiji cha Igogo.
“Kwa hiyo tunashirikiana na serikali ya kijiji na Wilaya ya Igunga
kuhakikisha samaki wale wanalindwa ili wawanufaishe wananchi wote,”
alisisitiza Karumbeta.
Kwa mujibu wa Karumbeta wadau wao ni halmashauri za wilaya, mji na
manispaa zilizopo kwenye mikoa hiyo, alitumia fursa hiyo pia kuzitaka
zione umuhimu wa kufugaji samaki kwa kuwa hakuna tatizo la mbegu kama
ilivyokuwa awali.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanzugi, Abeli Nchimo alisema ili
kukabiliana na wavuvi haramu, serikali ya kijiji imejipanga kuwatumia
askari wa jeshi la jadi ‘sungusungu’ kufanya doria usiku na mchana
katika bwawa hilo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment