Na Mwandishi wetu
Wizara
ya Mifugo na Uvuvi kanda ya kati imewaagiza watu wote
wanaojishughulisha na uvuvi haramu kwenye bwawa la Mwanzugi,lililopo
katika Kijiji cha Mwanzugi,wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora usiofuata
taratibu zilizowekwa waache mara moja na kwamba endapo wataendelea
kukaidi amri hiyo halali hatua kali na za kisheria zitachukuliwa dhidi
yao.
Afisa
Uvuvi Mfawidhi na uvunaji wa viumbe hai Kanda ya kati,Bwana Renatus
Charles Karumbeta alisema hayo katika mahojiano maalumu na mwandishi wa
gazeti hilo kufuatia malalamiko kwamba licha ya bwawa la Mwanzugi
kufungwa lakini bado kuna baadhi ya wavuvi kwa kushirikiana na maafisa
uvuvi wanaokwenda kuvua nyakati za usiku.
Aidha
Bwana Karumbeta alifafanua kwamba uvuvi haramu ni kuanzia kutokuwa na
leseni pamoja na kuvua samaki wadogo,hivyo kwa kushirikiana na
Halmashauri ya wilaya ya Igunga wamejipanga kuhakikisha kwamba wavuvi
wote wanavua katika eneo hilo wanafuata taratibu na kwamba hawatakuwa
tayari kukukabaliana kuruhusu uvuvi haramu uendelee katika wilaya hiyo.
Alifafanua
afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia ufugaji samaki katika mikoa ya
Dodoma,Singida na Tabora kuwa idara hiyo imeshaanza zoezi la kupandikiza
samaki na kwamba mpaka sasa jumla ya vifaranga 22,000 vya samaki katika
bwawa la Kijiji cha Igogo vimekwishapandikizwa.
“Kwa
hiyo tunashirikiana na serikali ya Kijiji pamoja na serikali ya wilaya
ya Igunga kuhakikisha kwamba samaki wale wanalindwa ili waweze
kufaidisha wananchi wote wa eneo zima”alifafanua zaidi Karumbeta.
Hata
hivyo afisa Mfawidhi huyo alisisitiza kwamba serikali wilayani Igunga
haitakubali kikundi kidogo cha watu ambao hawataki kufuata taratibu
kuharibia jamii nzima kwa sababu wanajua uvuvi au ufugaji wa samaki ni
vitu ambavyo vinakwenda pamoja.
Alisema
pamoja na kifaranga kimoja kuzalishwa kwa shilingi mia tatu lakini
serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi imeweza kupunguza bei ili
wananchi wengi waweze kununua na kila kifaranga kitauzwa kwa bei ya
shilingi mia moja.
Kwa
mujibu wa Bwana Karumbeta kwa kuwa wanawategemea wadau wao wakubwa kuwa
ni Halmashauri za wilaya,Mji na Manispaa zilizopo katika mikoa ya
Dodoma,Singida na Tabora alizishauri kuanza kuona umuhimu wa ufugaji wa
samaki kwa sababu hivi sasa hakuna tatizo la mbegu lililokuwa
likiwakabili hapo awali wananchi wa mikoa hiyo.
“Kituo
hiki kinatarajiwa kutoa vifaranga vya samaki laki mbili kila mwezi kwa
hiyo tunaomba Halmashauri,Taasisi mbali mbali na watu binafsi waje
kwenye kituo hiki kujifunza namna ya ufugaji bora wa samaki”.alifafanua
Bwana Karumbeta.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mwanzugi,Bwana Kusweka
Kaswenye alitumia fursa hiyo kuiomba wizara ya kilimo na ushirika kwa
kushirikiana na serikali ya wilaya kuhakikisha wakulima wa aina hiyo
wanadhibitiwa kikamilifu kwa madai kuwa uharibifu unaofanywa na wakulima
hao ni mkubwa zaidi kuliko ule unaofanywa na wavuvi haramu.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanzugi,Bwana Abeli Nchimo alisema ili
kukabiliana na wavuvi haramu serikali ya Kijiji hicho imejipanga kwa
kutumia askari wa jeshi la jadi,”Sungusungu”kufanya doria usiku na
mchana katika bwawa hilo.
Chanzo: Mo Blog
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment