Home » » BARAZA LAPINGA UKATILI

BARAZA LAPINGA UKATILI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

BARAZA la watoto wenye walemavu mkoani Tabora, limeitaka Serikali
kuwachukulia hatua kali wazazi wanaowaficha watoto wenye ulemavu
ikiwemo kuwafikisha mahakamani wauaji wa Albino.

Tamko hilo limetolewa na baraza hilo wakati likizungumza na vyombo vya habari juzi, na kuonesha kusikitishwa na unyama unaoendelea kufanyika kila siku dhidi yao.
Akisoma hotuba, mwenyekiti wa baraza hilo, Gloria John alisema linaundwa na halmashauri tatu za mkoa wa Tabora za Nzega, Sikonge na Tabora Manispaa chini ya usimamazi wa Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT).
Alisema licha ya kuanzishwa kwa baraza hilo, wao kama watoto wenye
ulemavu, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika maisha yao
ya kila siku.

Alizitaja kuwa ni pamoja na jamiii kuwa na mtazamo hasi dhidi ya watoto wenye ulemavu ndani ya familia zao kwa kisingizio kuwa ni balaa, mkosi na laana.
Gloria ambeye pia ni mlemavu wa macho, alisema watoto wenye ulemavu hutelekezwa na wazazi wao wa kiume kuhofia kuchekwa na kufedheheshwa na  jamii inayomzunguka.
Naye Said Shabani mtoto wa shule ya wasioona ya Furaha ambaye ni mlemvu
wa ngozi (albino), alisema watoto walemavu hawashirikishwi katika
maamuzi mabalimbali kwenye familia na ngazi nyingine za serikali ikiwa
ni pamoja kutengwa wakati kula na kulala.

Alisema hawapatiwi haki za msingi kama elimu na kuwa na miundombinu rafiki kwenye majengo ya umma, shule, vyoo, madarasa, vyombo vya usafiri sanjari na uhaba wa walimu wenye taaluma ya ulemavu.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora, Kudra Mwinyimvua, alisema ni jukumu la serikali kuhakikisha mkoa unakuwa na mabaraza ya watoto wenye ulemavu  sanjari na kushirikiana na asasi mbalimbali kama makanisa na mashirika ya serikali na yasiokuwa ya kiserikali.
Mchangaji Isaya Ilumba wa FPCT alisema kanisa linaelewa umuhimu
wa watoto wenye ulemavu kwani mlemavu ni mtu kama watu wengine.

Chanzo:Tanznia Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa