Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Wilaya ya Sikonge, mkoani Tabora kati ya Agosti Mosi hadi Oktoba 17 mwaka huu, imepokea malalamiko saba ya tuhuma za rushwa.
Kamanda wa Takukuru Wilaya ya Sikonge, Manyama Tungaraza, alieleza hayo kwenye taarifa yake katika kikao cha baraza la madiwani wilayani humo.
Alitaja malalamiko hayo kuwa ni watendaji wa vijiji na kata, polisi, mahakama, ushirika, fedha, mgambo na afya.
Alisema kati ya malalamiko hayo, manne uchunguzi wake unaendelea na uko kwenye hatua nzuri, wakati malalamiko matatu yamehamishiwa katika idara nyingine kwa ajili ya kushughulikiwa.
Mbali na hayo, alisema Takukuru wilaya imeendelea kuimarisha vilabu vya wapinga rushwa katika baadhi ya shule za sekondari kwa kutoa semina kwa wanafunzi na walimu
chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment