Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKOA wa Tabora umevuka lengo la kampeni shirikishi ya chanjo ya surua, rubera na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumembele licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Tabora, Dk. Elisha Ndakama, alisema lengo la kutoa chanjo hiyo limefikia asilimia 101 Mkoa wa Tabora.
Alisema zoezi hilo lililofanyika toka Oktoba 18 hadi 24 mwaka huu, watoto waliopata chanjo ya surua na rubera ni 1,191,690 sawa na asilimia 101 wakati lengo lilikuwa ni watoto 1,183,788.
Alisema kati ya watoto hao, wa kiume walikuwa ni 663,302 na wa kike 748,743.
Dk. Ndakama, alisema zoezi la kutoa dawa na kinga tiba hasa kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, waliopapatiwa chanjo hizo ni 1,387,198 sawa na asilimia 67 ya lengo la kuwapatia watu 2,065,711.
Alisema kati ya hao, watu wazima wanaume walikuwa ni 658,142 wakati wanawake ni 743,488.
Hata hivyo, Kaimu Mganga Mkuu huyo, alisema zoezi hilo liligubikwa na changamoto mbalimbali kutokana na imani potofu kuwa dawa hizo ni mpango ‘Freemason’ hali iliyosababisha watu wengi wasijitokze kumeza dawa ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Changamoto nyingine, alisema ni kushindwa kujitokeza kwa wanaume kupata dawa za kumeza kwa ajili ya kuzuia matende maji na mabusha, ambayo ni magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Dk. Ndakama, amewataka wananchi kuacha imani potofu kuwa dawa za kinga tiba zinazuia uzazi, bali zinatibu mabusha, matende na minyoo tumbo.
Aidha, alisema ubovu wa barabara na ukosefu wa watumishi lilikuwa ni tatizo kubwa katika utekelezaji wa zoezi hilo, lakini kutokana na jitihada za Wizara ya Afya na Ustwi wa Jamii, waliweza kufanikisha zoezi hilo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment