Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKOA wa Tabora umeandikisha jumla ya watoto 53,581 wa elimu ya awali katika mwaka wa masomo 2016.
Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia elimu
mkoani Tabora, Juma Mhina. Alitoa taarifa hiyo katika kikao cha wadau wa
elimu cha hivi karibuni, kilichoshirikisha maofisa kutoka halmashauri
zote saba za mkoa huo.
Alisema idadi hiyo ni ya watoto wote walioandikishwa katika
halmashauri zote za mkoa huo. Idadi halisi ya watoto waliotarajiwa
kuandikishwa ni 74,773 .
Alisema wavulana walioandikishwa ni 21,664, sawa na asilimia 57.6 na wasichana ni 21,917 sawa na asilimia 58.9.
Jumla ya watoto wote walioandikishwa katika wilaya zote ni 53,581,
sawa na asilimia 71.6. Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa
kuvuka lengo la makisio yake, ambapo watoto waliotarajiwa kuandikishwa
ni 4,881, lakini walioandikishwa ni 5,099 sawa na asilimia 104.5.
Akizungumzia uandikishwaji watoto wa kuanza darasa la kwanza, Mhina
alisema mkoa huo umefanikiwa kuandikisha jumla ya watoto 64,642 sawa na
asilimia 70.6 wakati matarajio ilikuwa kuandikisha watoto 91,506.
Alipongeza halmashauri ya Manispaa Tabora kwa kufanikiwa kuvuka lengo
la uandikishaji, ambapo iliandikisha watoto 7,644 sawa na asilimia 110
wakati matarajio yalikuwa kuandikisha watoto 6,924.
CHANZO: HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment