Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKOA wa Tabora umeshika nafasi ya mwisho katika matokeo ya wanafunzi
waliohitimu elimu ya msingi kwa mwaka jana, hali inayoonesha kushindwa
kwa wahusika wa elimu kufikia malengo waliyojiwekea kuhakikisha ufaulu
unapanda.
Inaelezwa kuwa, viongozi wa elimu mkoani hapa walikaa Januari 29,
mwaka jana kujadili mikakati ya kupandisha ufaulu kwa shule za msingi
kwenye mkoa huo, jambo lililoshindwa kuonesha mafanikio chanya katika
matokeo ya wanafunzi waliomaliza shule ya msingi mwaka huo.
Mkuu wa Mkoa, Ludovick Mwananzila alisema, ana imani kuwa
yaliyoazimiwa katika kikao hicho hayakufanyiwa kazi kikamilifu ndio
maana mkoa huo umeshika nafasi ya mwisho Tanzania Bara, katika matokeo
ya shule ya msingi.
“Nilijiuliza maswali mengi sana baada ya kupata matokeo, kulikuwa na
sababu gani ya kuitisha mkutano wa wadau na kuweka maazimio lukuki kwa
lengo la kuinua kiwango cha elimu na kuongeza ufaulu wa watoto wetu,
inaonesha kuna maazimio hayakufanyiwa kazi ipasavyo,” alisema.
Aidha, alibainisha kuwa kitendo cha mkoa huo kufanya vibaya katika
matokeo hayo kimechangiwa na Halmashauri za mkoa huo kushindwa kufanyia
kazi maelekezo yaliyotolewa katika vikao husika, ikiwemo kutosimamia
vizuri elimu. Aidha, aliwalaumu wakaguzi wa shule kushindwa kufanya kazi
yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kushindwa kufuatilia endapo walimu
wanafundisha au la.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment