Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora kimewataka viongozi wake
kufanya kazi za chama na kuacha kufanya kampeni za kuelekea uchaguzi wa
ndani utakaofanyika mwaka 2017.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Hassani Wakasuvi alisema hayo katika uzinduzi
wa sherehe za kuzaliwa kwa chama hicho zilizofanyika katika Kijiji cha
Busondo, Kata ya Puge Wilaya ya Nzega, kuwa baadhi ya viongozi wameacha
kufanya kazi za chama na kujikita kufanya kampeni za uchaguzi.
Akitaja ngazi za nafasi ambazo zinahangaika kufanya kampeni ni pamoja
na nafasi ya balozi wa nyumba kumi, mwenyekiti wa matawi, wenyeviti wa
kata, wenyeviti wa wilaya pamoja na yeye mwenyewe kwa nafasi yake
wanapaswa kufanya kazi kwani muda wa uchaguzi haujafika.
Alisema baadhi ya viongozi wameanza kuwa na hofu ya kuendelea na
nafasi zao, lakini wanapaswa kujikita kufanya kazi za chama bila
kuegemea upande wowote ili kuepusha makundi yanayoweza kukigharimu chama
hicho.
CHANZO : HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment