Jiografia:
Wilaya
ya Tabora inapatikana katika vipimo vya latitude 4°52' na 5°9' Kusini
na Longitude 32° 29' na 33° 00' Mashariki. Eneo kubwa la Wilaya lipo
kati ya mwinuko wa meta 1,000 na 1,500 juu ya usawa wa bahari. Wilaya ya
Tabora imezungukwa na Wilaya za Uyui upande wa Magharibi, Kaskazini na
Mashariki. Upande wa Kusini Tabora inapakana na Wilaya ya Sikonge.
Wilaya inayo Halmashauri moja ambayo ni Manispaa ya Tabora, na hiyo
ndiyo Makao Makuu ya Mkoa wa Tabora.
Utawala:
Wilaya
inazo tarafa 2, Kata 25 ambapo 13 kati ya hizo zipo mjini na 12 zipo
nje ya mji; vijiji 30, Vitongoji 116 na Mitaa 118. Wilaya inayo
Halmashauri moja tu yenye hadhi ya Manispaa.
0 comments:
Post a Comment