Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
29 .5.2017
Katibu
Tawala Mkoa wa Tabora Dkt .Thea Ntara ameuagiza uongozi wa Manispaa ya
Tabora na Maafisa Biashara kuhakikisha wanawaondoa haraka
wafanyabiashara wote waliotundika nguo za mitumba katika miti kwa ajili
ya kuuza na kufanya mji kuonekana mchafu.
Dkt. Ntara alitoa agizo hilo jana mjini Tabora wakati wa kikao na Wakuu wa Idara wa Ofisi yake.
Alisema
kuwa hivi sasa mji unaonekana mchafu kwa sababu ya baadhi ya
wafanyabiashara wa nguo za mitumba katika mitaa mingi ya Manispaa hiyo
kuamua kuweka bidhaa zao katika miti kama mahali rasmi pa kufanyia
biashara hiyo.
Dkt.Ntara
aliongeza kuwa ni vema Uongozi wa Manispaa ya Tabora wakahakikisha
wanatenga maeneo maalum ya vijana hao kuendesha kazi zao badala ya
kuwaacha wafanyebiashara kiholela katika maeneo yasiyo rasmi.
“Haiwezekani
kila mahali kwenye miti kunageuzwa sehemu ya kuuzia mitumba …ni lazima
mji ukae katika utaratibu na mpangilio unaofaa” alisema Katibu Tawala
huyo wa Mkoa.
Alisisitiza kuwa miti iliyopo mitaani ni kwa ajili ya kusaidia kutunza mazingira na kusaidia kivuli kwa wapita njia na sio ya kupanga na kuuzia nguo za mitumba.
Katika
hatua nyingine Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora ameuagiza Uongozi wa
Manispaa hiyo kutenga haraka eneo la kuchimba vyoo kwa ajili ya
wafanyabiashara wa Mnada wa eneo la Ipuli ili kuzuia watu kusaidia ovyo
katika eneo hilo.
Alisema
kuwa kama watashindwa kutekeleza agizo hilo atalazimika kusimamisha
shughuli za biashara ili kuzuia uwezekano wa kuzuka magonjwa ya mlipuko
kama vile kipindupindu ambayo yanaweza kusababisha maafa.
Dkt.
Ntara alisisitiza kuwa haiwezekana huduma mbalimbali kama vile uuzaji
wa vyakula, nyama choma na bidhaa nyingine zikafanyika katika eneo
ambalo halina huduma ya vyoo kwa ajili ya watu wanakwenda kununua na
kuuza bidhaa mbalimbali.
Alitoa
wiki moja kuhakikisha zoezi hilo linafanyika la sivyo hatachukua hatua
ya kusimamisha shughuli katika eneo hilo hadi hapo watakapoboresha na
kujenga vyoo.
0 comments:
Post a Comment