NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
21 November 2017
SERIKALI
imepiga marufuku Halmashauri zote nchini kuingia makubaliano na
Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’S) bila kupitia na kiuhidhinishwa
na Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa( TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa hayazingatia vipaumbule vya Serikali na kuokuwa na manufaa kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni mkoani Tabora na Naibu
Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za
Mikoa( TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na Watendaji na watumishi wa Mkoa huo.
Alisema kuwa mashirika
hayapaswi kuanza kazi katika Halmashauri yoyote kabla ya mpango kazi
wao hajaonwa na viongozi wa TAMISEMI ili kujidhirisha kama kweli malengo
yao yanaendana na vipaumbele vya Serikali vya kuboresha maisha ya
watanzana Watanzania ambao maisha yao yako chini.
Nzunda alisema baadhi ya mashirika hayo yamekuwa yakidai kusaidia Watanzania ,lakini matokeo yake ni kuwanufaisha viongozi wa mashirika hayo na wachache.
“Kwa
mfano Mashirika hayo yanapokuja kutaka fulani kama vile elimu ni vema
yakajua kuwa vipaumbele vya Serikali …….mfano kuboresha miundo mbinu ya
kujifunzia na kufundishia, kuwajengea uwezo walimu, kuwepo na vifaa vya
kufundishia na kuweka mazingira mazuri kwa watoto wenye mahitaji
kujifunza na kusoma katika mazingira rafiki” alisema Nzunda
Alisema
kuwa wanapoaandika taarifa kwenda kwa watu waliowawezesha fedha
wanaonyesha kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo ya
mabilioni ya fedha kumbe sio kweli fedha nyingi zimeshia mifukoni kwa
wachache na unapoenda katika eneo ambalo wanadai kusaidia hakuna kitu.
Nzunda
alisema kuwa Serikali inelenga kuhakikisha kuwa kama fedha zinatolewa
kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia eneo husika na kama wafadhili
wanapokuja waone kuwa fedha waliotoa imefanya kazi inayoonekana na sio
maelezo yasiyo na ushahidi.
Alisema
kuwa Serikali inapenda kushirikiana na wadau mbalimbali lakini ni vema
wadau hao watambue kuwa vipo vipaumbele ambavyo inavikusudia katika
kuwaletea maendeleo watu wake.
Katika
hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo ameagiza kuwa majengo yote
yanayojengwa katika Shule na Taasisi mbalimbali za elimu yawe rafiki kwa
watu wenye mahitaji maalumu na watoto wa kike ili kuondoa vikwazo vya
wao kupata elimu.
Alisema
kuwa baadhi ya majengo yamekuwa yakisababu wanafunzi wenye mahitaji
maalumu kushindwa kuhudhiria masomo yao vizuri na kukwamisha ndoto zao
za kuapata elimu.
Nzunda
alisema kuwa yapo majengo ambayo yamekuwa hayana maeneo mazuri kwa
ajili ya watoto wa kike na kuwafanya washindwe kuhudhuria masomo katika
kipindi Fulani cha mwezi.
0 comments:
Post a Comment