Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
NA TIGANYA VINCENT, RS-TABORA
SERIKALI imepiga marufuku Halmashauri zote nchini
kuingia makubaliano na Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali(NGO’S) bila kupitia na
kiuhidhinishwa na Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa(
TAMISEMI ) kwa kuwa baadhi ya mambo yamekuwa hayaendebi na vipaumbule vya
Serikali ambayo nakusudia kuwasaidia kuwasaidia wananchi.
Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Naibu
Katibu Mkuu (ELIMU) Ofisi ya Rais , Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa(
TAMISEMI ) Tixon Nzunda wakati akizungumza na Watendaji na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Tabora, Manispaa ya Tabora , Halmashauri za Wilaya ya Sikonge, Uyui , Kaliua na
Urambo.
Alisema kuwa
kabla ya kuanza utekelezaji wa shughuli za NGO ni vema Halmashauri
zikapeleka maombi ya mashirika ambayo yameomba kufanyakazi katika maeneo yao ili
Serikali inone kama kweli inaendana na vipaumbele ambavyo imepanga katika kuboresha
maisha ya watanzana ambao maisha yao yako chini.
Nzunda alisema mashirika hayo yamekuwa yakidai pesa
ya kusaidia Watanzania kutoka kwa wafadhili lakini matokeo yake fedha hizo
zimekuwa zikiishi kuwanufaisha watu wachache na wanapoaandika taarifa kwa watu
waliowapa fedha wadai kuwa wamewasaidia Watanzania katika miradi ya maendeleo
ya mabilioni ya fedha kumbe sio kweli imeshia mifukoni kwa wachache.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inelenga
kuhakikisha kuwa kama fedha zinatolewa kwa ajili ya walemgwa ziende kusaidia
eneo husika ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana kwa jami husika , kwa
Serikali na wafadhili na wafadhili husika.
Nzunda alisema kuwa kumekuwepo na mashirika ambapo
yamekuwa yakutumia mbinu ya kuwasaidia wananchi kumbe fedha hizo zimekuwa
zikiwanufaisha watu wachache kwa kulipwa posho na mambo mengine ambayo hayana
tija kwa wananchi wa kawaida.
Alisema Mashirika amabayo yana nia ya kweli ya kusaididia
watanzania lazima yakubaliane na viapumbe vya Serikali ili yaweze kufanya
kufanya kazi nchini vingine ni vema yakatafute nchini nyingine ya kufanya mambo
yake bila kufuata utaratibu wa nchi hisika.
Nzunda alitoa wito kwa Halmashauri ya kuhakikisha
kuwa kabla ya kuyaruhusu Mashirika hayo yamepata kibali cha TAMISEMI ili
kuepuka kisingizio cha kuwageuza wananchi mtaji wa wache kujipatia fedha kwa
maslahi binafisi.
Alisema mashirika yamekuwa yakianda taarifa nzuri
kwa wanawapa fedha kuwa wamesaidia jamii husika kumbe hakuna kinachoonekana Zaidi
ya wao kunufaika
Nzunda alisema kuwa Halmashauri itakayoingia makubaliano ya
NGO bila kupitia TAMISEMI watendaji wake itabika wawajibishwe kwa kusimamia
maslahi ya umma.
Naibu Katibu Mkuu yupo katika ziara ya kikazi
katika Mikoa ya Kigoma, Tabora na Singida kwa lengo ya kuhimiza usimamizi bora
wa sekta ya elimu , kilimo, mifugo , utawala bora na mengine mengi.
0 comments:
Post a Comment