WAKAZI
Mkoani Tabora wametakiwa kulima mazao ya korosho na mihogo kwa ajili
kujiongezea kipato ambacho kitawawezesha kuboresha maisha yao na
kujiinua kiuchumi.
Kauli
hiyo imetolewa jana wilyani Uyui na Waziri wa Kilimo Dkt. Charles
Tizeba wakati alikwenda kuangalia maandalizi ya kilimo cha zao hilo na
kampeni za uhamasishaji wananchi kulima kwa wingi zao hilo
zinazoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
Alisema kuwa mazao hayo pia yatawasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi kwa sababu yanahitajika sehemu mbalimbali duniani.
Dkt. Tizeba alisema kuwa hivi sasa zao la korosho linabei nzuri na ndilo limeongoza kwa kuingiza fedha za kigeni hapa nchini.
Alisema
kuwa wakulima wote wanaohitaji kulima zao hilo ni vema wakajiandikisha
kwa Maofisa Kilimo wa Wilaya kwa ajili ya kupata michezo ya zao hilo.
Waziri
huyo aliongeza kuwa katika hekta miche inayohitajika ni 27 hadi 33 na
inaanza kuvunwa baada ya miaka mitatu na wakulima wataendelea kufaidika
kwa kipindi cha miaka 50 ijayo baada ya upandaji.
Alisema
kuwa hivi sasa wakati wa maeneo ya Pwani maisha yao yamekuwa mazuri kwa
sababu ya zao hilo na kuongeza kuwa ni fursa kwa wakazi wa Tabora
kuanza kulima zao hilo.
Dkt.
Tizeba aliwaeleza wakazi wa Tabora kuwa tayari Serikali imeshaleta
mbegu za korosho mkoani humo kwa ajili ya wakulima ambao wako tayari
kulima zao hilo kuanza kupanda.
Kuhusu zao la Mhogo alisema kuwa hivi sasa linahitajika sehemu mbalimbali duniani la kulifanya kuwa zao la biashara.
Alisema
kuwa udongo wa Tabora unastawi mihogo ni vema wakatumia fursa hiyo
kulima kwa wingi na hasa mbegu inakabiliana na ugonjwa mbalimbali.
Alisema kuwa nchi mbalimbali zimekuwa zikiitaji mihogo na hivyo kutoa fursa kwa zao hilo kuwa la biashara.
Dkt.
Tizeba aliwaagiza Maofisa Ugani kuwasaidia wakulima kupata mbegu za
mihogo ambazo zinazokabiliana na ugonjwa kutoka katika Chuo cha Kilimo
Tumbi na maeneo mengine ili wakulima waweze kuchamkia fursa hiyo kwa
ajili ya kuboresha maisha yao na kuleta fedha za kigeni.
Kwa
upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa mkoa huo
umeamua kulima kwa wingi mazao kama vile korosho, pamba, tumbaku ,
alizeti na mazao mengine yakiwemo ya chakula kwa ajili ya kupata
malighafi za kutosha kwa ajili ya viwanda vilivyopo na
vitakavyoanzishwa.
Alisema
kuwa kwa upande wa alizeti kila familia itapaswa kulima ekari mbili kwa
ajili ya kuwa na mazao ya kutosha ambayo yatawavutia wawekezashaji
katika Kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment