Home » » TAARIFA: WATU 16 WAMEFARIKI KATIKA AJALI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA NA WENGINE 75 KUJERUHIWA

TAARIFA: WATU 16 WAMEFARIKI KATIKA AJALI WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA NA WENGINE 75 KUJERUHIWA


Na Mwandishi Wetu, Tabora
Watu   16 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 750 kujeruhiwa  baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji  cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
Ajali hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda  Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.
Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.
Pia inadaiwa kuwa madereva wa mabasi hayo wamefariki huku yule wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe akiwa amekatika kiwiliwili na  kuwa jitihada za kutafuta kichwa  chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi( Day-worker)
na mwendo kasi na imeelezwa kuwa  karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwataja walikufa kuwa ni 17 pamoja na majeruhi hao 75 na kuwa Polisi wanafanya uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo.
Baadhi ya miili ya marehemu.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

1 comments:

Anonymous said...

SO SORRY FOR THEM

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa