Home » » Kasulumbayi: Jiandikisheni kwa wingi

Kasulumbayi: Jiandikisheni kwa wingi


na Mustapha Kapalata, Nzega
WANANCHI wilayani hapa mkoani Tabora wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura pindi wakati utakapowadia.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Sylivester Kasulumbayi alisema hayo katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) uliofanyika wilayani hapa.
Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kutambua haki zao kwa nyakati tofauti sambamba na kuwaepuka baadhi ya watu watakaopita na kuzorotesha zoezi hilo.
Alizitaja faida za kujiandikisha katika daftari hilo ni pamoja na kupata fursa ya kupiga kura pamoja na kukitumia kitambulisho hicho kwa matumizi mbalimbali ya kijamii na ya kiserikali.
Pamoja na mambo mengine, aliwatahadharisha wananchi hao kuvihifadhi vitambulisho hivyo kwa umakini ili kuhakikisha wanapata nafasi ya kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2015, na pia vijana kushiriki kikamilifu katika chaguzi bila kukosa.
Naye Joseph Kashindye aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo Igunga kupitia chama hicho, aliwataka wananchi hao kuiunga mkono CHADEMA katika harakati mbalimbali za kuweza kuleta ukombozi.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa