Home » » CCM YAPITISHA JINA LA NAIBU MEYA

CCM YAPITISHA JINA LA NAIBU MEYA

na Hastin Liumba, Tabora
MCHAKATO wa kumpata naibu meya wa Manispaa ya Tabora, umeanza kupamba moto baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitisha jina la mgombea wake ambaye ni Diwani wa Kata ya Ipuli, Waziri Mlenda.
Uchaguzi huo wa CCM ulikuwa na wagombea wanne, ambapo wawili; Hadija Nkumba wa Kata ya Uyui na Haruna Kulwa wa Kata ya Itetemia, walijitoa kabla ya uchaguzi kuanza.
Kujitoa kwa wagombea hao, kuliwabakiza kwenye kinyang`anyiro Diwani wa Kata ya Ipuli, Mlenda na Juma Makala wa Kata ya Ifucha.
Idadi ya madiwani waliopiga kura kwenye uchaguzi huo ni 32 ambapo kura 24 zilimchagua Mlenda na kura nane zilikwenda kwa Makala.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mlenda alisema jina lake sasa litapelekwa katika uchaguzi wa Baraza la Madiwani ambapo anatarajia kupambana na mgombea wa CHADEMA.
Mlenda alisema endapo atafanikiwa kupata nafasi hiyo, atahakikisha makundi yaliyopo yanamalizwa kwa manufaa ya halmashauri hiyo.
"Nikifanikiwa kupata nafasi hiyo, nitamaliza makundi na hali hiyo itasaidia kujenga manispaa iliyo bora na usimamizi makini,” alisema.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa