Home » » DIWANI AAHIDI USHIRIKIANO UVCCM TABORA

DIWANI AAHIDI USHIRIKIANO UVCCM TABORA

Mwandishi wetu, Tabora
Diwani wa kata ya Nata wilaya ya Nzega mkoani Tabora, Joseph Kulwa Malongi, amejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya makamo mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM Taifa katika uchaguzi mkuu wa jumuiya hiyo unaotarajia kufanyika oktoba mwaka huu.
Malongi, alichukua fomu hiyo katika ofisi ya CCM mkoani Tabora, ambapo aliahidi kutoa ushirikiano madhubuti kwa vijana na kutojihusisha na siasa za makundi ambazo alisema hazina tija kwa umoja huo wala faida kwa chama cha Mapinduzi.
Amesema kuwa kutokana na mtazamo wake ni vyema vijana wakatambua uwepo wa matatizo yao na kuweka mikakati ya kupambana nayo ambapo alisema mojawapo ya kikwazo kikubwa kwa vijana ni namna ya kujikwamua kiuchumi hivyo baadhi yao wakijikuta wakitumiwa katika makundi.
Wakati ambapo Diwani huyo akichukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo, mmoja wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Nzega, Edfoce Fredrick Rwangisa, naye amechukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi ya mjumbe wa Baraza kuu la Umoja wa vijana wa CCM Taifa, kupitia mkoa wa Tabora.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa