Na Abdallah Amiri, Igunga
WATU wasiojulikana wamechoma moto ghala la pamba katika Kijiji cha Ipumbulya, Kata ya Bukoko Wilaya ya Igunga mkoani Tabora. Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Charles Lucas, tukio hilo lilitokea Agosti 8, mwaka huu, saa nane usiku.
Alisema akiwa nyumbani kwake aliona moto ukiwaka katika ghala hilo, linalomilikiwa na Kikundi cha Imalaupina kilichopo kijijini hapo.
Alisema juhudi za wananchi kuuzima moto huo zilifanikisha kuokoa baadhi ya pamba kidogo iliyokuwamo ndani ya ghala hilo.
Katibu na Meneja wa Kikundi cha Imalaupina, Mihangwa Kodinelo, alisema pamba iliyoungua ni kilo 16,591 yenye thamani ya Sh 10,950,060 iliyonunuliwa kutoka kwa wakulima.
Alisema mlinzi wa stoo hiyo, Issa Ernest (32), alitoroka baada ya tukio hilo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu, alisema kuungua kwa pamba hiyo kutadhoofisha maendeleo ya wananchi.
Aliwataka Polisi wilayani humo kumsaka mlinzi huyo hadi apatikane na afikishwe katika vyombo vya sheria.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment