Sunday kabaye, Tabora
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatma Mwassa, amewataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora, Kurudisha kiasi cha shilingi milioni 850 zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambazo wamezitumia kulipana posho.
Mkuu wa mkoa alitoa kauli hiyo alipokuwa kwenye ukaguzi wa ujenzi wa zahanati ya Kitunda wilyani Sikonge, ambapo alisema amesikitishwa sana na hali halisi aliyoikuta katika zahanati ambapo jengo ni zuri lakini wagonjwa wanaendelea kuteseka kwa kutumia vitanda vibovu.
Alisema haiwezekani watanzania wakaendelea kuteseka na kuumia kwa kulala katika vitanda vibovu wakati serikali imetoa fedha kwa ajili ya kuendeleza utoaji wa huduma za afya kwa jamii ambayo viongozi wanakaa na kujilipa posho bila ya kuwa na huruma kwa wananchi.
Ninawaagiza kuanzia sasa ni marufuku kutumia pesa zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia miradi ya maendeleo kwa umma, kutumiwa kwa ajili ya kulipana posho na hivyo kudidimiza maendeleo yanayotaka kupelekwa kwa wananchi.
Sitaki kusikia mmelipana posho na kwamba nawaagiza asilimia 25 ya pesa hizi zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa zahanati zimetumiwa kulipana posho katika vikao mbali mbali ikiwemo vikao vya kawaida vya kamati ya afya ya wilaya.
Mapema Mkuu huyo wa mkoa alipokeaa tarifa kutoka kwa mkandarasi kuhusu sababu zilizopelekea ujenzi wa zahanati hiyo kuchelewa na hivyo kusababisha kiwango cha ukarabati kilichotarajiwa kutofikiwa kwa haraka huku mkandarasi katika utekelezwaji wa mradi huo akionekana kuwa goi goi.
Baada ya ukaguzi huo Mkuu wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuzungumza na wananchi wa kitunda na kuwaeleza jinsi Rais Jakaya Kikwete alivyotekeleza aahadi yake ya kutoa gari la wagonjwa katika tarafa ya Kitunda na kuahidi pia kuendelea kushirikiana nao ili kuhakikisha kwamba maendeleo ya tarafa hiyo yanapatikana.
0 comments:
Post a Comment