Mwandishi wetu, Tabora
Wakuu wa kaya nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanaandaa orodha ya majina ya watu wote watakaolala katika kaya zao usiku wa agosti 25 mwaka huu ili orodha hiyo iwasaidie kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa.
Wito huo umetolewa na mhamasishaji wa zoezi la sensa ya watu na makazi nchini, Said Ameir, alipokuwa kwenye mahoajiano mafupi na waandishi wahabari kuhusu utaratibu wa kuhesabu watu katika zoezi hilo utakavyoendeshwa.
Alisema kulingana na sheria na utaratibu wa kuhesabu watu siku hiyo itakuwa ni kila mtu atahesabiwa katika nyumba aliyolala usiku huo na siyo vinginevyo, jambo ambalo alisema wakuu wa kaya wanapaswa kulitambua na kuliandaa ili waweze kutoa taarifa sahihi.
Alisema iwapo kama kaya itakuwa imepatwa na janga kama msiba ama arobaini basi mkuu wa kaya hiyo atawajibika kupata taarifa sahihi za watu watakaolala katika kaya yake na kisha taarifa hizo kutolew kwa karani wa sensa atakayewajibika kuhesabu watu katika eneo husika.
hata hivyo alionya kuwa atakayeshindwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani wa sensa atashitakiwa kwa mujibu wa sheria na kwamba kama akipatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha mpaka miaka 2 jela ama kulipa faini.
Said, amesema kuwa pia iwapo kama itagundulika kuwa karani wa sensa ametoa taarifa za siri za sensa kwa watu wasiohusika anaweza kuhukumiwa kifungo kama hicho jela ama kulipa faini isiyozidi shilingi 100,000.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment