Home » » CHAMA CHA MSINGI USINDI HATARINI KUFA‏

CHAMA CHA MSINGI USINDI HATARINI KUFA‏



Na Hastin Liumba,Kaliua
 
CHAMA CHA MSINGI USINDI HATARINI KUFA
 
CHAMA msingi cha Usindi kata ya Ushokola wilaya ya Kaliua mkoani
Tabora  cha wakulima wa zao la Tumbaku kiko mbio kukumbwa na mgogoro
miongoni mwa wanachama wake na uongozi hali inayotishia uhai wa chama
hicho chenye wanachama zaidi ya 400.
 
Makamu mwenyekiti wa chama cha msingi Usindi Mikidadi Mustafa alisema
hayo wakati akifanya mahojiano na gazeti hili kijijini humo.
 
Mustafa anasema chanzo cha kuishi kwa uhasama kijijini hapo
kumesababishwa na kundi dogo ambalo lina watu 18 waliofukuzwa ndani ya
chama kwa kuikuka taratibu,kanuni na sheria za ushirika.
 
Anasema hivi sasa hali siyo nzuri hapa kijijini kwani wapo
waliojeruhiwa kwa risasi,walipigwa baruti na waliovamiwa na kuporwa
fedha,waliwekewa sumu na kuporwa pikipiki hadi leo hakuna
aliyekamatwa.
 
Aidha makamu mwenyekiti huyo anasema hivi sasa kutokana na uhasama huo
huwenda hali ya uzalishaji kijijini hapo ukashuka kwani imefikia
mahali watu wanshindwa kuandaa mashamba kutokana na kukatishwa tamaa
na kundi dogo linaloendesha vitendo vya kikatili.
 
Makamu mwenyekiti huyo aliongozana na katibu meneja wake Johakimu
Herman na mhasibu Mohammed Abdalah alisema hadi sasa kijijini hapo
kumechomwa mabani tisa ya kukaushia tumbaku yenye thamani ya sh
milioni 5.4.
 
Aidha alisema licha ya kuchomwa mabani hayo vitalu vya kuoteshea mbegu
za tumbaku vilifyekwa na kupaliliwa vikiwa na thamani ya sh 720,000.
 
Pamoja na uongozi wa chama cha msingi kuingilia kati na kutoa taarifa
kituo cha polisi Kaliua bado hali ni mbaya huku kukiwa na vitisho
mbalimbali.
 
Alisema licha ya kuwepo kundi dogo la watu wanaoendesha ukatili pia
wapo wachache wengine ambao waliruhusu waganga wa kienyeji wajulikanao
kama “Kamchape” na baada ya mkuu wa wilaya ya Kaliua Saveli Maketa
kukemea na kupiga marufuku watu hao ambao wanafahamika walikasirishwa
na kufanya vurugu na vitisho.
 
Makamu mwenyekiti huyo alisema chama hicho hadi sasa kina wanachama
400 wanachama hao wamefikia mahali wamekata tamaa hasa kutokana na
wachahe wanaofanya hujuma za kuchoma mabani na wengine wamekuwa
wakifyeka vitalu vya mbegu za tumbaku hali inayowakatisha tamaa.
 
“Fikiria ndugu yangu mwandishi unaingia gharama za kukopa pembejeo
hala unaotesha miche ya tumbaku unaaamka asubuhi na kukuta watu
wasiojulikana wamefyeka ama kung`oa miche hiyo unafikiri msimu ujao
kilimo kitakuwaje.”alisema.
 
Aidha waliongeza kuwa imefikia mahali sasa katika kijiji cha Usindi
wananchi wanaishi katika makundi mawili kwani kuna kundi moja
linamsapoti na kumuunga mkono mwenyekiti wa serikali ya kijiji Haji
Said na jingine ambao ni wakulima wamebaki kama watoto yatima kutokana
na kutuhumiwa vibaya.
 
Alisema chuki iliyopo pale kijijini kwao pia inatokana na baadhi ya
wakulima kupunjwa dola kwa msimu wa 2010/2011 japokuwa walilipwa kwa
mbinde.
 
Hata hivyo baadhi ya wakulima waliofukuzwa kwenye chama cha msingi
kati ya 18 walisema uongozi huo una majungu na wamekuwa wakisingizia
mambo mengi ya kuzusha.
 
“Toka tumelipwaa mapunjo ya dola msimu wa 2010/2011 mwenyekiti wa
chama cha msingi Usindi Hassan Magola anawachongea kwa mwenyekiti wa
kijiji Haji Said ambaye naye anapandikiza majungu kwa mkuu wa wilaya
kuwa wao ni majambazi na wahamiaji haramu.” walisema.
 
Naye kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Peter Ouma alisema hana taarifa
hizo ila alihaidi kuzifanyia kazi taarifa hizo ikiwemo kundi la
waganga wa kienyeji maarufu kama Kamchape.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa