ALIYEKUWA Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Urambo, mkoani
Tabora, Oscar Bulugu, anayekabiliwa na tuhuma tatu za kuomba na kupokea
rushwa amekutwa na majalada zaidi ya 30 nyumbani kwake.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa mkoani Tabora, Fidelis Kalungura, ilileleza hakimu huyo
alipekuliwa na maofisa wa TAKUKURU na kukutwa na majala 31 ya kesi
mbalimbali.
Kalungura alisema TAKUKURU ilifanya upekuzi nyumbani kwa Hakimu
Bulugu baada ya wananchi kupeleka malalamiko ya mara kwa mara wakidai
kutotendewa haki na Mahakama ya Wilaya ya Urambo.
Katika malalamiko yao, wananchi walidai wanapofika mahakamani hapo
wanakosa huduma kwa kuwa majalada ya kesi zao hayaonekani kwa makarani.
Kutokana na malalamiko hayo TAKUKURU ilifanya uchunguzi na
walipokwenda kupekua nyumbani kwa hakimu huyo walikuta majalada hayo.
Habari kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Tabora
zimethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba aliishasimamishwa kazi
kwa mujibu wa sheria.
Aprili mwaka huu TAKUKURU mkoani hapa ilimkamata na kumfikisha
mahakamani Hakimu Bulugu kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya sh
milioni tano.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment