MRADI wa ujenzi wa
daraja la mbutu wilayani Igunga mkoani Tabora ambao unatarajia kugharimu zaidi
ya shilingi billion 13 mpaka kukamilika mapema mwaka 2014 unatarajiwa kuwa
chachu ya maendeleo.
Katibu mkuu wa umoja
wa wanawake Tanzania amefanya ziara ya kushitukiza katika mradi huo ili
kujionea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha mapinduzi (CCM) huku
akiwataka vijana wanaofanyakazi katika mradi huo kuwa wazalendo.
Mhe. Amina Makilagi
ambae ni Katibu wa umoja wa wanawanake Tanzania anawasili hapa kujionea ujenzi
wa daraja la mbutu wilayani Igunga ambao unatarajiwa kukamilika kuwa chachu ya
maendeleo ya wananchi na kuepusha vifo ambavyo vimekuwa vikijitokeza nyakati za
masika katika mto huu.
Katibu huyo akiwa
ameambatana na viongozi wengine wa kitaifa wa Jumuia hiyo pamoja na viongozi wa
mkoa wa Tabora anabainisha madhumuni ya ziara yake kuwa taarifa za kwenye
karatasi sinzuri kama kufika katika eneo la mradi na kujua maendeleo.
Hapa katika utekelezaji wa
mradi wa ujenzi wa daraja la mbutu nao kijana Adam Jumanne amesema wanatoa wito
kwa vijana wenzao wanaoshinda vijiweni kuja kufanyakazi hapo kwani na fasi
zipo.
Kwa upande wake mwakilishi wa
Mbunge wa jimbo la Igunga Mariamagdalena Kafumu, amesema kukamilika kwa ujenzi
huo kutawaondolea kero wananchi ya muda mrefu ambayo ikiwa ni pamoja na
kusombwa na maji nyakati za msimu wa mvuas.
Katika ziara hii ya
Katibu mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania wilayani hapa pamoja na ujumbe wake
wamesisitiza uzalendo na amani ili kuyafikia maendeleo ya kweli.
0 comments:
Post a Comment