ALIYEKUWA
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo Mkoani Tabora Oscar
Bulugu, anayekabiliwa na tuhuma tatu za kuomba na kupokea Rushwa
amejikuta matatani baada ya kukutwa akiwa na majalada ya Kesi zaidi ya
Thelathini nyumbani kwake.
Taarifa
iliyotolewa na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani
Tabora, Fidelis Kalungura, imeeleza kuwa Hakimu huyo alipekuliwa na Maafisa wa
TAKUKURU na kukutwa na majalada yapatayo Thelathini na Moja ya kesi mbali
mbali.
Kalungura
aliongeza kuwa TAKUKURU ilichukua jukumu la kufanya upekuzi nyumbani kwa
Hakimu Bulugu baada ya wananchi kupeleka malalamiko ya mara kwa mara wakidai
kutotendewa haki na Mahakama ya Wilaya ya Urambo.
Katika
malalamiko yao wananchi wamekuwa wakidai kuwa wanapofika Mahakama ya Wilaya ya
Urambo wanakosa huduma kwa kuwa majalada ya kesi zao hayaonekani kwa
makarani kwa vile yapo kwa Hakimu aliyesimamishwa.
Kufuatia
malalamiko hayo TAKUKURU iliamua kufanya uchunguzi wa kina na baada
ya kujiridhisha walienda kupekua nyumbani kwa Hakimu huyo na kukuta akiwa na
majalada hayo
Mwezi
Aprili mwaka huu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,(TAKUKURU),Mkoani
hapa ilimkamata na kumfikisha Mahakamani Hakimu mkazi mfawidhi huyo,Oscar
Bulugu kwa tuhuma tatu za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni tano.
Hakimu
Bulugu Katika kesi yake inayomkabili anatuhumiwa kuwa alitenda makosa
hayo kati ya Mwezi Machi 15 mwaka huu hadi Machi 22 huko wilaya ya Urambo
akiwa ni Hakimu Mkazi Mfawidhi.
Katika
kesi hiyo upande wa mashitaka ulidai kuwa Machi 15 mwaka huu mtuhumia akiwa ni
Hakimu wa wilaya ya Urambo alimshawishi Lucas Raymond Changala ampe fedha
hizo ili kumpa dhamana ndugu yake aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya wizi wa
fedha za benki ya NMB.
Mwanasheria wa TAKUKURU katika shauri hilo, Simon Mashindia, alidai katika shtaka la pili kuwa tarehe 18 Machi Mwaka huu hakimu huyo ambaye ni mtuhumiwa alipokea shilingi milioni moja toka kwa Changala kama malipo ya awali ili aweze kumpa dhamana Phillipo Raymond aliyekuwa mtumishi wa benki ya NMB tawi la Urambo anayetuhumiwa kuiba zaidi ya shilingi milioni mia moja.
Mwanasheria huyo wa TAKUKURU alidai katika shitaka la tatu kuwa tarehe 21/03/2013 mtuhumiwa huyo alipokea tena shilingi milioni moja ikiwa ni endelezo la malipo aliyoomba aweze kumpa dhamana mtumishi huyo wa NMB tawi la Urambo
0 comments:
Post a Comment