Serikali imeitaka Kampuni ya Ujenzi ya Chaines Construction and
Communication inayojenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Nzega Mjini
hadi Puge, kuhakikisha kuwa inakamilisha kazi hiyo ndani ya miezi saba.
Agizo hilo lilitolewa juzi na Waziri wa Ujenzi, Dk
John Magufuli alipokuwa akizungumza na wananchi wa Nzega baada ya
kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika mradi huo mkubwa.
Alisema mkandarasi huyo katika barabara hiyo yenye
urefu wa kilomita 68, anafanyakazi kwa kusuasua tofauti na Wakandarasi
wa naojenga kipande cha Barabara cha kati ya Tabora-Puge na yule wa
Tabora-Urambo.
Alisema kitendo cha kufanyakazi hiyo kwa kusuasua kinasababisha wananchi kuuliza maswali mengi kwa viongozi wao.
Kauli hiyo ya Dk Magufuli ilikuja baada ya wananchi kulalamikia maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Wananchi hao walisema hawajapendezwa na kasi ya
ujenzi wa kipande hicho cha barabara na kwamba kuna haja ya kuchukua
hatua dhidi ya mkandarasi, ili kazi hiyo ikamilike haraka.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment