Na Hastin Liumba,Igunga.
MVUA kubwa iliyoambana na upepo mkali imeezua mapaa ya nyumba na mtu
mmoja kupoteza maisha katika kata ya Choma wilaya ya Igunga mkoani
Tabora.
Mvua hiyo ambayo ilinyesha jana imesababisha maafa makubwa katika
kata hiyo huku zaidi ya kaya kumi zikiwa hazina mahali pa kuishi.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisa mtendaji wa kata ya Choma
Ntemi James alisema kuwa mvua hiyo ambayo ilikuwa imeambatana na upepo
mkali ilinyesha kwa zaidi ya masaa mawili.
Alisema kuwa kufuatia mvua hiyo nyumba zaidi ya kumi ziliezuliwa paa
pamoja na paa la kanisa moja la TAG lililopo katika kata hiyo
kuanguka.
Aliongeza kuwa mtu aliyepoteza maisha kwa kuangukiwa na jengo la
kanisa hilo ni Vumilia Luhende(15) mkazi wa kata hiyo ya Choma.
Alisema kuwa watu wengine watano walijeruhiwa katika jengo hilo la
kanisa ambao ni Agnes Nhyemde(18),Scolastika Sengerema(18),Mary
Shija(15),Christina Dohoi(15) pamoja na Mchungaji wa kanisa hilo John
Mdimi(53)wote wakazi wa kata ya Choma.
Aidha Ofisa mtendaji huyo alisema kuwa kufuatia maafa hayo pia vitu
mbalimbali vilihalibiwa na kuongeza kuwa thamani ya vitu vyote
vilivyohalibiwa ni jumla ya Tsh.4,293,000/=.
Nae Diwani wa kata ya Choma Peter Onesmo alisema kuwa watu ambao
hawana makazi kutokana na kuezuliwa kwa nyumba zao wamehifadhiwa kwa
majirani huku kamati ya maafa ya kata hiyo ikitafuta jitihada zingine
za kuwasaidia.
Kwa upande wake mratibu wa kamati ya maafa wilaya ya Igunga Marco
Kapela alisema kuwa kamati ya maafa ngazi ya wilaya inajipanga
kuchukua tahadhali dhidi ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha katika
msimu huu wa masika.
Home »
» MMOJA APOTEZA MAISHA, KAYA ZAIDI YA KUMI WAKOSA MAKAZI KUFUATIA MVUA KUBWA.
0 comments:
Post a Comment