Na Hastin Liumba,Tabora
SERIKALI mkoa wa Tabora,imesema haitakuwa tayari kusikia wananchi
wanalalamikia huduma mbovu za matibabu kwa kadi (TIKA) wakati
walishachangia fedha.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatma Mwassa alitoa angalizo hilo kwenye kikao
cha wadau wa uanzishaji wa mfuko wa afya ya jamii (TIKA) iliyofanyika
mkoa hapa.
Mwassa alisema ikiwa huduma bora zitakuwepo vituo vya kutolea huduma
ambavyo vipo chini ya halmashauri hatutahitaji kutumia nguvu nyingi
katika kuhamasisha.
Alisema halmashauri ihakikishe huduma zinzkuwa bora kwenye vituo vyote
ikiwemo lugha nzuri kwa wanachama upatikanaji wa dawa kwa wingi na
vifaa tiba.
Mkuu huyo wa mkoa aliongeza kuwa halmashauri itakusanya fedha
zitokanazo na michango ya wanachama na baadaye itahitaji kuomba fedha
za tele kwa tele kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya.
Aliongeza asilimia 67 za fedha za michango ya wanachama pamoja na zile
za tele kwa tele ni lzima zitumike kununulia dawa na kuhakikisha
muongozo wa matumizi ya fedha unafuatwa kikamilifu.
Aidha aliongeza kuwa mfuko huo una manufaa kama uwezo wa uchangiaji wa
wananchi lakini wamuazi wakubwa wa mpango huu juu ya viwango vya
uchangiaji ni wadau wa kikao hicho kwa siku hiyo.
Alisema utaratibu huu ni wa hiari lakini hiari hiyo ni ya uwajibikaji
ambapo mwananchi anapaswa kulipia kiasi kitakachoamuliwa na baada ya
hapo anapaswa kupata matibabu yenye haki.
Mwassa aliongeza kuwa mwananchi yoyote aliyelipia mamlaka inapaswa
kuhakikisha wananchi waliolipia wanapatiwa matibabu kutokana na
michango yao.
Alisema utaratibu huu siyo mgeni kwani zipo halmashauri zilizopata
mafanikio makubwa na kuweza kuboresha huduma za matibabu kutokana na
mapato yatoakanayo na mfuko huu.
Alitolea mfano halmashauri za Igunga,Kahama na Iramba zimefanikiwa
kununua dawa,kajiri watumishi wa muda kumalizia vituo vya afya na
kufanya ukarabati wa vyombo vya usafiri hiyo ni kutokana na wananchi
wengi kuchangia kutokana na kuona umuhimu wake.
Home »
» SERIKALI YATAKA HUDUMA ZA TIKA ZIWE NA TIJA.
0 comments:
Post a Comment