Home » » ASKARI WA JWTZ KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

ASKARI WA JWTZ KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

ASKARI wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora kwa tuhuma ya kumpiga hadi kumuua Chacha Juma, mkazi wa Nzega Mjini.
Akisoma mashitaka hayo mwendesha mashitaka Melito Ukongoji, alisema mbele ya Hakimu Mkazi Joseph Katikilo Ngomero kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Agosti 27 mwaka huu katika mgodi wa dhahabu wa Resolute uliopo wilayani Nzega.
Waliofikishwa mahakamani hapo ni sajini Omary Idd (46) askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na Anderson Mweisingwa (33) wa Suma JKT.
Melito aliendelea kuiambia mahakama hiyo kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja walimpiga Chacha Juma mpaka kumsababishia kifo chake.
Hata hivyo Hakim Mkazi Joseph Katikilo Ngomero aliwataka watuhumiwa kutojibu kitu chochote kwani mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo hadi litakapo fikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Chanzo;Habari Leo 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa