Home » » WALIMU KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA VYETI

WALIMU KIZIMBANI WAKIDAIWA KUIBA VYETI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WALIMU watatu wa Shule ya Sekondari Badri iliyoko wilayani Nzega, Tabora wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora kwa mashitaka ya wizi wa vyeti viwili vya wanafunzi.
Wanadaiwa kuiba cheti cha Elias Kabate na Daniel Makorobelo waliohitimu Kidato cha Nne mwaka 2011 katika shule hiyo. Vyeti hivyo ni vilivyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Melito Ukongoji aliwasomea mashitaka mwishoni mwa wiki mbele ya Hakimu Mkazi, Joseph Ngomero.
Alitaja walimu hao ni Adamu Maziku (58) mkazi wa Nzega , Emmanuel Chaba (33) mkazi wa Nyasa Nzega pamoja na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Mkoba Chaba (45).
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka, Machi 3, mwaka juzi, katika Shule ya Sekondari Badri walimu hao waliiba vyeti vya wanafunzi hao vilivyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania kwa kuhitimu elimu ya Kidato cha Nne.
Mwendesha Mashitaka alidai walitenda kosa hilo wakifahamu ni kinyume na kifungu cha sheria 273 (b) ya kanuni ya adhabu sura ya 19 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Aliomba Mahakama iahirishe kesi kutokana na upelelezi kutokamilika. Washitakiwa walikana mashitaka na wako nje kwa dhamana. Kesi iliahirishwa hadi Septemba 3, mwaka huu.
Chanzo;Habari Leo 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa