Home » » MADIWANI NZEGA WALIA NA WANASIASA

MADIWANI NZEGA WALIA NA WANASIASA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
MADIWANI wa Halamashauri ya Wilaya ya Nzega mkoani Tabora, wametaka wanasiasa kutoingiza siasa kwenye miradi ya maendeleo.
Baadhi ya madiwani waliyozungumza na Tanzania Daima mara baada ya kuwasilisha taarifa za miradi ya maendeleo ya kata zao kwenye baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya Nzega, walisema wanasiasa wamekuwa tatizo kwenye miradi hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari, madiwani hao walisema kutokamilika kwa wakati na uwepo wa miradi isiyoridhisha, kunatokana na baadhi ya wanasiasa kuingiza makundi ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Walisema wapo wanasiasa wanaingiza makundi ya uchaguzi kwenye miradi ya maendeleo ya wananchi, ikiwa ni kwa maslahi na makundi yao, hali ambayo inachangia miradi hiyo kuzoroteshwa.
Aidha, waliongeza kuwa miradi hiyo pia inakwama kutokana na wananchi waliyo wengi kutotambua na kuwa na uelewa mdogo juu ya uchangiaji kwenye miradi.
Madiwani hao, wanasema wananchi wengi wamekuwa wakitegemea sana kuegemea serikali au halmashauri kutoa fedha kwenye miradi ya maendeleo.
Hata hivyo, madiwani hao walitoa wito na ushauri kwa kuomba wanasiasa kuacha kuingilia watalaamu kwenye miradi ya maendeleo.
Aidha, madiwani hao waliwageukia watalaamu na kuwataka kuacha tabia ya kupenda kuomba asilimia kumi (Ten Percent), wakandarasi ili kuwe na miradi inayokamilika kwa wakati na iliyo bora.
Chanzo;Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited : |
Copyright © 2012. Tabora Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa