Baadhi ya majengo ya Mahakama za Mwanzo Mkoa wa Tabora
yamechakaa na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha ya wananchi
wanaokwenda kupata huduma kwenye mahakama hizo na hata wafanyakazi wake.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Tabora,
Wilfred Dyansobera aliyataja majengo yanayohatarisha maisha ya wananchi
na wafanyakazi wake kuwa ni pamoja na yale ya maeneo ya Urambo, Kigwa,
Ussoke, Igalula, Sikonge, Ichemba, Isevya na Goweko.
Akizungumza na gazeti hili kuhusu utoaji wa huduma
katika Mahakama hizo jana, Naibu msajili huyo alisema, watendaji wa
Mahakama hizo wanajitahidi na akiwahimiza wananchi kuhakikisha
wanazifahamu haki zao na wakati huohuo kuzisaidia Mahakama kutimiza
wajibu wake.
Amewaasa pia watumishi wa Mahakama Kanda ya
Tabora, kuzingatia maadili ya kazi zao na akionya mwananchi kupewe
huduma baada ya kuinunua na kudai kuwa hilo ni kosa na ni kinyume cha
sheria na taratibu zilizowekwa.
Naibu msajili huyo alisema mtumishi wa Mahakama
ana wajibu wa kutoa huduma kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo
iliyowekwa na kwa muda mwafaka.
Alisema iwapo mtumishi wa mahakama atabainika
kutoa huduma kwa kuomba rushwa atakuwa ametenda kosa la jinai na
aliyeombwa anaruhusiwa kwenda sehemu nyingine kudai haki itendeke kama
Takukuru au Polisi ama kwa mwajiri wake.
Alisema iwapo itathibitika hatua zinaweza kuchukuliwa zikiwamo za kinidhamu kama vile kusimamishwa au kufukuzwa kazi.
Dyansobera alisema iwapo kila upande utafahamu
haki na wajibu wake taswira ya Mahakama katika jamii haitachafuka
anaamini kuwa Mahakama ni chombo cha kukimbilia kila mtu iwe Serikali au
mtu binafsi.
na kwamba lazima iaminiwe na kila mdau anayepewa huduma na chombo hicho.
ChanzoMwananchi
ChanzoMwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment